Kishindo... Kishindo ... Kongamano kubwa la usomaji wa Qur-ani kwa Tajweed latikisa Jijini la Tanga.

24 Mei 2025 - 18:38

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-  Hadhira Jijini Tanga, washangazwa sana na usomaji wa kipekee wa Tajweed na wa kustaajabisha, wenye naghma za kupendeza na unaoambatana na sauti nzuri zisizo za kawaida.

Maajabu | Kongamano kubwa la Qur'an Tukufu: Mji wa Tanga Wazizima

Msomaji: Rajai Ayoub awachanganya wakazi wa Jiji la Tanga. Uwanja mzima ulisimama wima kwa Furaha na kushangilia kwa kukoshwa na Usomaji wake Maridhawa... namaanisha kwamba watu wote walisimama kwa kustaajabu huku wakipiga Takbir kwa nguvu.

Maajabu | Kongamano kubwa la Qur'an Tukufu: Mji wa Tanga Wazizima

Maajabu | Kongamano kubwa la Qur'an Tukufu: Mji wa Tanga Wazizima

Msomaji: Anko Idi naye kwa upande wake akawachanganya kabisaa kupitia mapito yake Maridadi ya Usomaji wa Qur'an.

Makundi kwa makundi waliamua kuvamia jukwaa baada ya kuvutiwa na sauti yake maridadi, kupelekea ashindwe kuendelea kusoma na badala yake Anko Idi  akaendelea kulia kwa kitambo kirefu, huku makundi kwa makundi wakiendelea kumiminika kwenye jukwaa la kusomea.

Maajabu | Kongamano kubwa la Qur'an Tukufu: Mji wa Tanga Wazizima

Naam! Juhudi za kuwatuliza wapenzi wa Qur'an zikafanikiwa baada ya kitambo na kulazimika kutumia nguvu ili warudi majukwaani.

Yallah! Zingatia walinzi walikuwa hawakujiandaa kushuhudia tukio kama hili ambalo awali liliwafanya wapigwe na butwaa kwa dakika kadhaa wasijue la kufanya.

Maajabu | Kongamano kubwa la Qur'an Tukufu: Mji wa Tanga Wazizima

Shakir Najad kutoka Iran | Ni Hatari

Bwana huyu Shakir Najad, Msomaji mahiri sana na Bingwa kutoka Nchini Iran akaja kusema kivitendo kwamba:

"Haya mambo siyo kwamba tunayaweza, bali ni asili na utamaduni wetu na yapo kwenye damu zetu...."

Inabidi unielewe kwamba bwana mkubwa huyo alianza kama masihara hivi...  kidogo kidogo ... ghafla macho yangu yakashuhudia watu wengi wanakimbia kutoka kila upande kuelekea kwenye jukwaa la kusomea ambalo lilikuwa katikati ya uwanja.

Nimekubali msomaji huyo ana uzoefu mkubwa sana. 

Ndiyo....  Ana uzoefu....

Kwa sababu wavamizi ambao walimsonga huku na kule, waliokuwa wanakanyagana huku wakipiga kelele kubwa za Takbir, kamwe hazikukatisha mpango wake wa kuendelea kuonyesha ufundi mkubwa wa Kusoma Qur'an mbele ya halaiki.

Maajabu | Kongamano kubwa la Qur'an Tukufu: Mji wa Tanga Wazizima

Allah!.. Yaani Karim 

Kongamano hilo linafanywa kwa ushirikiano wa BAKWATA, JMAT, Kituo cha Utamaduni cha Iran na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustwafa (s) - Tawi la Tanzania.

Hili ni Kongamano la pili, na kesho Jumapili Kongamano la tatu litafanyika Viwanja vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam.


Tanbihi:

Habari hii imekujieni kwa hisani kubwa ya:

Dr. Harith Nkussa - Msemaji Maalum wa Mufti wa Tanzania.
Jumamosi 24.5.2025.

Your Comment

You are replying to: .
captcha